Kwa zaidi ya miaka 30, chama cha wataalamu shirika la madaktari mbadala "Freie Heilpraktiker e.v." imekuwa ikisimamia mahusiano ya kijamii na kujishughulisha na utaalamu wa madaktari mbadala kwa njia mbalimbali. Tunatoa taarifa, ushauri, mafunzo na kuandaa kongamano, maonesho na makundi ya kikanda.Tunaendesha mahusiano makubwa ya umma kwa ajili ya wataalamu wa udaktari mbadala. Tunajitolea katika sera za udaktari na utaalamu sambamba na athari katika jamii, na tumejotolea kwa niaba ya wagonjwa na wafanyakazi kwa ujumla. Tunatoa taarifa zenye ukweli na zilizofanyiwa utafiti wa kina kwa vyombo vya habari na siasa.Wagonjwa wanaweza kupata taarifa zaidi kuhusu taaluma hii na namna inavyofanya kazi na tunasaidia upatikanaji wa madaktari mbadala walio katika maeneo ya ukaribu ya aliyopo mgonjwa. Kama unamuamko wa kuwa daktari au kupata mafunzo ya matibabu mbadala utapata taarifa muhimu, ushauri na semina za kuvutia mbalimbali pamoja nasi. Tunafanya kazi pamoja na mashirika mengine katika shughuli za muhimu zinazohusu muingiliano na masuala ya kitaaluma.